Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya wakazi wa mji wa Kisii wamekosa amani kutokana na uvundo ambao unatoka kwenye mfereji wa maji chafu ambayo imepasuka katika sehemu ya mji huo.

Wakiongea siku ya Jumatatu na Mwaandishi huyo katika steji ya magari yanayofanya kazi ya teksi karibu na jengo la Uhuru Plaza mjini humo, wakazi hao walisema hawana amani katika kazi yao kwa kuwa uvundo unaotoka katika mfereji wa maji hayo machafu umesababisha mazingira kuwa na harufu mbaya mno.

“Uvundo unaotoka kwenye mifereji hiyo ni ya harufu mbaya mno na tumekosa amani katika biashara zetu kwani hata wateja kukaribia mahali hapa ni shida kubwa kwa sababu ya uvundo huo,” alihoji Jonnes Obao, mhudumu wa teksi mjini Kisii.

Kwa sasa wameiomba idara husika kuharakisha na kusaidia kurekebisha mfereji hiyo kwani hata magonjwa huenda yakatokea mjini Kisii kutokana na hali hiyo mbaya ya mazingira.

“Tunaiomba idara husika kutusaidia na kurekebisha mfereji hiyo ili nasi tuwe na mazingira masafi kila wakati,” alihoji Gerison Mosige, mkazi mwingine.

Kwa mujibu wa wakazi hao wamekuwa wakiripoti visa hivyo kwa Gusii Water and Sanitization Company(Gwasco) lakini bado hawajashughulikiwa.

“Tuna uoga wa kuwa katika mazingira haya machafu kwani uvundo huu huenda ukasababisha magonjwa mbalimbali kwetu," aliongezea Mosige.

Kwa upande wa idara husika wakiongozwa na mwnyekiti Evans Bosire, tayari wameweka mikakati kabambe ya kurekebisha mfereji hiyo ili kutatua shida hiyo inayoleta uvundo huo.