Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa eneo bunge la Bochari kaunti ya Kisii wana kila sababu ya kutabasamu baada ya mkuu wa idara ya afya katika Kaunti ya Kisii Sarah Omache kuaahidi kuwa hospitali ya Iyabe itapanuliwa.

Upanuzi wa hospitali hiyo unanuwia kuimarisha huduma ya matibabu katika hospitali hiyo.

Akizungumza siku ya Jumatatu katika hospitali hiyo ya Iyabe, wakati mbunge wa eneo bunge hilo Zepedeo Opore alifadhili hospitali hiyo 'generator' ambayo itawasaidia kuendeleza huduma za kutibu wakati nguvu za umeme zimepotea, Sarah Omache alisema mikakati kabambe imeimarishwa na Kaunti ya Kisii ili hospitali hiyo ipanuliwe zaidi.

Wakati huo huo, mbunge Opore aliahidi kushiriakiana na serikali ya kaunti kujenga hospitali hiyo huku akitumia hazina ya ustawi maeneo bunge jinsi alivyoahidi hapo mbeleni wakati serikali za ugatuzi zilikuwa bado hazijaanzishwa na kusema lazima atimeze ahadi hiyo.

“Hospitali hii ya Iyabe itabanuliwa zaidi na tutaipandisha mpaka iwe level Four ili huduma za matibabu ziimarishwe kikamilifu zaidi na wananchi wa sehemu hii wafurahie huduma ya matibabu,” alisema Omache.

Aidha, mbunge Opore alisema atajenga chumba cha akina mama ambacho watakuwa wakitumia wakati wanajifungua maana chumba hicho hakiko kwa sasa jambo ambalo liliwafurahisha wakazi wa eneo hilo.

“Nitajenga chumba ambacho akina mama watakuwa wakijifungulia ili wasisumbuke kusafiri katika hospitali ya rufaa ya Kisii kwani ni mbali,” alisema Opore.