Mwanasiasa mmoja kutoka Kisii amewataka wenzake kumcha na kulieneza neno la Mwenyezi Mungu badala ya siasa ya kila siku wanapopata umati.
Mwakilishi wa Wadi ya Kiogoro iliyoko Kaunti ya Kisii Alex Aboko aliwaomba wanasiasa wa eneo la Kisii kumhenzi Mwenyezi Mungu kabla ya kujiunga na maswala mengine yasiyo ya kimaendeleo.
Akiongea siku ya Jumanne katika eneo la Wadi ya Gesusu alipohudhuria mazishi ya nduguye mwanasiasa Hezekiel Ombaki wa Nyaribari Masaba, mwakilishi huyo aliwaomba wakazi wa Kisii kumweka Mola mbele ili Awaongoze kimaendeleo na katika shughuli yao ya kila siku.
Mwakilishi Aboko pia amewataka wananchi kuwasaidia na kushiriki katika baraza za maendeleo pindi tu wanapoharifiwa na viongozi wao.
"Sisi ni watumwa wenu na inatubidi kuitikia wito wenu kuwafanyia kazi lakini la maana ni kuwa lazima mshiriki nasi katika utaratibu wote unao lenga kuleta maendeleo katika eneo letu," alisema Mwakilishi Aboko.
Kiongozi huyo pia aliwataka vijana kuwa katika mstari wa mbele katika shughuli ya maendeleo wala sio kutumiwa na baadhi ya viongozi kwa manufaa yao binafsi. Alidai kuwa vijana wengi ndio chanzo cha kusorota na kukwama kwa maendeleo mengi katika eneo la Kisii kwa jumula.
Aliyehudhuria hafla hiyo pia ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Maseno Evans Onkarora aliyewataka viongozi kutotenga vijana katika shughuli za maendeleo na basi kuleta upinzani wakati maendeleo au miradhi zinapoanzinshwa.
"Viongozi wajumuishe vijana katika maendeleo ili kutoleta upinziani wakati wa kutekeleze miradhi humu nchini, vijana wametengwa sana wakati wa kupanga mikakati ya maendeleo hayo," alisema Profesa Onkarora.