Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Huenda shughuli za uchukuzi katika kivuko cha feri cha Likoni mjini Mombasa zikaimarika zaidi baada ya mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Musa Hassan kusema kwamba huduma za magari maalum yanayopita juu ya hewa kwa kutumia nyaya za umeme zitaanza Disemba mwaka ujao.

Akiongea na wanahabari siku ya Ijumaa baada ya mkatano na wadau wa kibiashara mjini Mombasa, Musa amesema kwamba hatua hiyo ya vigari hivyo vya kutumia nyaya za umme kutaboresha huduma katika kivuko hicho, sawa na kupunguza msongamo wa magari na abiria wanatumia kivuko hicho.

“Tumepanga mikati mwafaka ya kuimarisha shughuli za uchukuzi katika kivuko hicho licha ya kuwepo na changamoto lakini jihudi hizo zitafanikiwa. Wasimamizi wa kampuni ya huduma za feri imefanya majadiliano ya kina na serikali kuu, na shughuli hiyo tunatumaini kuanza rasmi mwaka ujao,” alisema Musa.

Kulingana na Musa, huduma hiyo haitakuwa sawia na ile ya sasa kwani watu watakaovuka wakitumia vigari hiyo watalazimika kulipa ada ya shilingi 20 ama 30, hali itakayopelekea kampuni hiyo kuimarisha huduma zake katika kivuko hicho.

“Kiwango cha fedha tumeweka cha shilingi 20 ama 30 kwa kila abiria sio kikubwa, tunatumani wananchi watashirikiana na wasimamizi wa kampuni hiyo na shughuli za uchukuzi katika kivuko hicho hazitakuwa tena na pingamiz,i” aliongeza Musa.

Musa amehoji kwamba huduma ya vigari hivyo maalum katika kivuko hicho cha Likoni huenda ikavutia watalii wengi zaidi kuzuru katika eneo la Pwani na kuimarisha sekta ya utalii iliyokumbwa na changamoto.