Share news tips with us here at Hivisasa

Idara ya utabiri ya hali ya hewa imetoa tahadhari kwa wakazi wa Pwani kujitayarisha kwa mvua kubwa kuanzia usiku wa Jumatano.

Kwenye taarifa iliyowekwa kwenye tuvuti ya idara hiyo, ukanda wa Pwani unatarajiwa kupokea mvua kubwa kuanzia mwezi huu hadi mwezi wa Disemba.

Maeneo ambayo mvua itanyesha zaidi ni Lamu, Malindi, Mombasa, Kilifi, Mtwapa, Msambweni na Lungalunga.

Kulingana na idara hiyo, sehemu zillizopokea mvua zaidi ya milimita 20 kwa siku kufikia sasa ni Marsabit na Moyale.

Jumatano Idara ya Ardhi na Nyumba Mombasa kupitia waziri wake Francis Thoya walibomoa ukuta unaozunguka jumba la kibiashara la Naivas liliko Kiembeni kwa sababu ya kuziba njia ya maji.

Serikali ya kaunti ya Mombasa itaendeleza ubomoaji wa majengo yanayoziba njia za maji.

Katika kaunti ya Taita Taveta afisaa mshrikishi wa kitengo cha kukabiliana na ukame Adam Kheri amewataka wakaazi kaunti hiyo kutumia fursa ya mvua hiyo ya El nino kuvuna maji watakayoyatumia nyakati ya ukame kunyunyiza mimea yao maji, sawia na kupanda miti.