Kamishna wa kaunti ya Nyamira Josphine Onunga ameombwa kuwaokoa wanafunzi wa shule wanaobugia pombe haramu wilayani Nyamira Kaskazini.
Wito huo umetolewa na wakazi wa eneo la Bomwagamo wilayani Nyamira kaskazini, ambao walidai kuwa pombe haramu imeongezeka pakubwa katika eneo hilo.
Wakazi hao walidai kuwa tangu shule zifungwe, wanafunzi wengi wamekuwa wakibugia pombe.
Wakazi hao wamesema pombe haramu wilayani Nyamira kaskazini imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kumtaka kamishena kuingilia kati na kukomesha shida hiyo.
Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumatatu katika eneo hilo la Bomwagamo, wakazi hao wakiongozwa na Peterson Orero walisema pombe imewaharibu vijana wa umri mdogo.
Walidai kuwa tangu mradi wa umwagaji pombe uanze nchini, machifu na baadhi ya maafisa wa polisi katika lokesheni tatu za Mageri, Mawekoa na Mabariri hawajakuwa wakitekeleza shughuli hiyo ya kumwagawa pombe.
Walimwomba Kamishna Onunga kuingilia kati na kukomesha ugema kama njia moja ya kuwaokoa vijana wao ambao wameonekana kupotelea kwa pombe.
“Tangu pombe ianze kumwagwa hakuna shughuli kama hiyo imetekelezwa hapa .Sisi tunaona wagema wa eneo hili wakiendelea na shughuli yao. Tunamwomba kamishna wetu Onunga atusaidie aokoe vijana ambao ni wa shule kabla hawajapotea kamwe,” alisema Beatrice Moseti, mkazi.
“Kama serikali inahitaji kukomeza pombe, kamishena wetu anapaswa kukuja eneo hili kwanza maana vijana waliofunga shule wameanza kubugia pombe haramu,” alisema Vincent Makori, mkazi.