Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wanachama wa vikundi vidogovidogo katika Kaunti ya Kisii wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali ya kaunti ya Kisii kukubali kuwakabidhi mikopo ili kujiendeleza kimaisha.

Haya yote yaliafikiwa siku ya Jumatano baada ya Mwakilishi wa wadi ya Magenche Timothy Ogugu kufikisha mswada katika bunge la Kaunti ya Kisii kwa jina ‘Kisii County Trade Scheme’.

Mswada huo uliopitishwa na idadi kubwa ya wawakilishi wa bunge hilo utahakikisha kuwa vikundi vyote vitakabidhiwa mikopo bila ubaguzi wowote.

Wafanyibiashara wa kaunti nzima ya Kisii nao wamepata afueni ya kupata usimamizi ulio mwema katika masoko mbalimbali ya kuendeleza biashara baada ya mswada wa wafinyibiashara hao kwa jina ‘Kisii County Credit Market’ kupitishawa.

Wafanyibiashara hao sasa watafurahia haki yao ya kufanya biashara. 

Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae atatia sahihi miswada hiyo ambayo ilipitishwa kuwa sheria rasmi katika Kaunti ya Kisii.