Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 30 ameponea chupuchupu baada ya kupigwa na nguvu za umeme na kurushwa kutoka ghorofa ya pili ya jumba.

Jackson Moriasi, alijipata katika hatari hiyo wakati alipokuwa akipaka rangi kwenye jumba moja lililoko katika eneo la Jogoo.

James Mokua ambaye alishuhudia tokeo hilo, alisema kuwa aliona mtu akianguka kutoka kwa ghorofa hilo na baadaye waliweza kubaini kuwa waya moja ambayo inaunganisha umeme katika jumba hilo iliweza kushika maji ya rangi.

“Mimi niliona mtu akianguka nikadhani alikanyaga mbao vibaya ikavunjika, kumbe ni nguvu za umeme. Kwa bahati nzuri hakufa,” alisema Mokua.

Bwana Alois Simba ambaye ni kiongozi wa wafanyi biashara wa maduka, aliiomba kampuni ya kusambaza umeme nchini tawi la Kisii kuhakikisha kuwa nyaya ambazo zimeunganishiwa hasa katika majumba makubwa ni thabiti.

Alisema kuwa baadhi ya nyaya hizo huenda zikasababisha mkasa mbaya zaidi zisipo angaliwa na kushughulika mapema.

Mwathiriwa aliweza kupelekwa katika kituo cha afya cha Oresi kufanyiwa matibabu.