Share news tips with us here at Hivisasa

Mwalimu mkuu wa shule ya kitaifa ya wasichana ya Asumbi dada Ann Josiphine Apiyo amewataka washikadau wote katika sekta ya elimu kuwapa wasichana nafasi ya kipekee katika maswala ya elimu.

Dada Apiyo alikuwa akiongea katika hafla ya siku ya elimu katika shule ya kitaifa ya wasichana ya Nyabururu katika Kaunti ndogo ya Kisii ya Kati.

Akiutubia umati uliohudhuria siku ya Ijumaa, dada Apiyo aliwasuta washikadau hao kutowapa wasichana nafasi ya kipekee katika maswala ya elimu nchini, pia aliwataka wakenya wote kuchukulia swala la elimu ya wasichana kuwa jambo la muhimu sana.

"Mkielimisha msichana, ni dunia nzima mmeelimishe na maisha ya wasichana na jamii nzima yatakuwa ya kutamani siku za mbeleni.," alisihi dada Apiyo.

Aidha, dada huyo aliwapa changamoto wasichana wote walio katika shule za upili katika Kaunti ya Kisii kuiga mfano wa wasichana wa shule yake ya Asumbi, ambao alisema mia moja miongoni mwao walipata alama ya A katika somo la hesabu.

Dada Apiyo pia alisema kuwa shule yake ya Asumbi yalenga kuimarisha matokeo yote ya sayansi na kuongeza kuwa wana lengo la alama ya kumi na moja katika mitihani ya kitaifa ya mwaka huu.

Shule ya wasichna ya Asumbi ilikua na alma ya A mia moja katika somo la hesabu katika mithiani ya kitaifa ya mwaka jana, mwaka huu wakiwa na lengo la kupata alama ya kumi na moja.

Mbunge wa eneo hilo la Kitutu Chache Kusini alizituza shule zilizofanya vyema kwa pesa, vitabu na vikombe huku akiahidi kuimarisha viwango vya elimu katika eneo hilo na kaunti ndogo ya Kisii ya Kati.