Wakulima kutoka sehemu ya Masaba kusini kaunti ya Kisii wamehimizwa kukuza zao la pareto ili kujiendeleaza kiuchumi.
Akiongea siku ya Alhamisi katika eneo la Masaba Kusini, soko la Masimaba, Mwenyekti wa mikopo ya serikali ya kaunti ya Kisii tawi la Baasi Samwel Matonda aliwahimiza wakulima wa eneo hilo kukuza zao hilo ambalo lina uhaba nchini.
Kulingana na Matonda, wakulima wengi wa eneo hilo wameeegemea sana ukulima wa mahindi na mazao mengine, na kulikwepa zao la pareto ambalo kwa wakati mmoja lilikua la muhimu.
“Pareto imepewa mgongo eneo hili letu na uchumi wa kaunti yetu hautaendelea tusipoanza kukuza zao la pareto, kumbuka kwa wakati mmoja zao hili lilitusaidia sana kama jamii na wengine wetu likawa ndio njia ya pekee katika ulipaji wa karo,” Matonda alisema.
Pia aliwaarifu wakaazi hao kuwa serikali, na haswa kaunti ya Kisii, ingali tayari kuwapa mbegu bila malipo ili kuanzinsha ukulima wa zao hilo.
Aliandamana naye mwanasiasa Benard Moseti, ambaye aliwahidi wakaazi hao kushirikiana nao hili kujiendeleza katika sekta ya kilimo.
“Tuko tayari kama viongozi kuwasaidia nyinyi kama wakulima ili pareto iwe ndio jinzi ya kujipatia riziki na muwafunze watoto wenu bila shida ya karo,” Moseti alidai.