Share news tips with us here at Hivisasa

Polisi wa eneo la Kikuyu waliweza kumwaga lita 200 ya pombe haramu katika eneo la King'ero na kuwatia mbaroni washukiwa wawili wanaodaiwa kutekeleza biashara hiyo haramu hapo siku ya Ijumaa.

Oparesheni hiyo ikiongozwa na Afisa mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kikuyu Inspekta Joshua Arende ilianza mapema siku ya Ijumaa walipovamia eneo hilo ambalo ni maarufu katika eneo la Kikuyu kwa kutekeleza biashara hiyo.

Maafisa wa Polisi wakisaidiana na machifu na naibu wao waliweza kumwaga pombe haramu aina ya 'chang'aa' lita 200 na kuweza kuwakamata washukiwa wawili ambao wanadaiwa kuwa wenye biashara hiyo.

Inspekta Arende akizungumzia kisa hicho alisema kwamba waliweza kunasa dumu 12 pamoja na meko ambazo zinatumika kutayarisha pombe hiyo haramu.

Alieleza kwamba washukiwa waliokamatwa wanasemekana kuwa wenyeji wa Limuru lakini biashara hii wanaitekeleza

katika eneo hilo akiongeza kwamba vita dhidi ya pombe haramu vitaendelea katika eneo hilo na zinginezo.

"Baada ya oparesheni iliyotuchukuwa takriban masaa manne, tunatumai kwamba biashara hii itakoma katika eneo hili, lakini bado tutaangazia macho yetu hapa na eneo zingine zote ili tuweze kumaliza biashara hii ya pombe haramu," alisema Afisa Arende.

Beth Wangari, mkaazi wa eneo hilo alisifu oparesheni hiyo akisema kwamba vita hivyo ni vya kusaidia vizazi vijavyo na kuokoa wale walio katika janga hilo.

Alisema kwamba polisi wasichoke kurudi katika eneo hilo kupambana na biashara hiyo ambayo alisema kuwa imeharibu maisha ya watu wengi, haswa vijana akiongeza kuwa biashara hiyo inaweza endelea pindi wanapojua polisi hawarudi. kufanya msako tena