Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Baada ya bunge la kaunti ya Nyamira kuwasimamisha kazi maafisa sita kwa madai ya utumizi mbaya na uvujaji wa pesa, Gavana wa kaunti ya Nyamira John Nyagarama amewarudisha maafisa hao sita kwenye wizara mbalimbali.

Maafisa hao walisimamishwa kazi kwa takribani miezi mitatu iliyopita kwa madai ya ufisadi. Kulingana na gavana Nyagarama, maafisa hao hawakuwa na makosa baada ya kuchunguzwa na kamati iliyoundwa hapo hawali na bunge la kaunti hiyo, jambo ambalo baadhi ya wabunge wa kaunti hiyo hawakukubaliana nayo.

Mnamo siku ya Jumatatu, gavana Nyagarama aliwarudisha maafisa hao kwenye wizara mbalimbali kando na zile walizokuwa wakiziwakilisha kabla ya kusimamishwa kazi.

Miongoni mwao ni Kepha Osoro, aliyekuwa katika wizara ya barabara, na sasa atawakilisha wizara ya mazingira na maji, John Omanwa aliyekuwa katika wizara ya pesa na sasa atawakilisha wizara ya biashara na utarii.

Andrew Ombati, aliyekuwa katika wizara ya mazingira sasa atakuwa katika wizara ya usimamizi kwa wananchi, Peter Omwanza alisalia katika wizara ya hapo awali ambayo ni ya vijana na michezo katika kaunti ya hiyo ya Nyamira.

Maafisa wengine wakuu waliorudishwa kazi ni Fridah Nyaboga, wizara ya Elimu, na Ernest Morara, masuala ya michezo.

Kamati mbili ziliundwa ili kuwachunguza maafisa hao sita kwa madai ya ufisadi, lakini kamati ya iliwaondolea maafisa wanne kati ya sita kutokuwa na makosa ya ufisadi, huku kamati nyengine iliwaondolea wote sita makosa ya ufisadi, jambo ambalo spika wa bunge la kaunti hiyo Joash Nyamoko alifutilia mbali kufuatia ripoti zao ambazo hazikuambatana,  lakini sasa imeafikiwa na gavana Nyagarama.