Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu Gavana wa kaunti ya Joash Maangi amekanusha madai ya kusema alipanga maandamano ya kumwaribia jina Gavana wa kaunti ya Kisii James Omariba Ongwae.

Akizungumza na waandishi wa habari  afisini mwake siku ya Jumatatu baada ya maandamano hayo Maangi alisema hakuhusika vyovyote kwa maandamano yaliyofanyika katika eneo la Ogemnbo.

Maandamano hayo yalifanywa na waendeshaji bodaboda kulalamikia uongonzi  wa Gavana Ongwae kwa kutotengeneza steji ya magari katika eneo hilo.

Aidha, Maangi alisema si vizuri watu kuingiza siasa kwa maandamano ya aina hiyo na kusema kuwa  hakupanga maandamano hayo jinsi wengi wanavyosema.

“Mimi  sikujua kuwa kuna maanadamano. Ninawaomba wale wanaoleta siasa kila wakati wakome maana hiyo ni njama ya kutaka kuvuruga uongozi wa Kaunti ya Kisii na kuniharibia jina,” alisema Maangi.

Jambo hilo la kusema kuwa Maangi ndiye aliyepanga maandamano hayo yaliwaacha wakaazi wengi vinywa wazi kwani Maangi ni kiongozi ambaye hufanya kazi na gavana Ongwae huku baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Kisii waliozungumza na waandishi wa habari jana kukerwa na jambo hilo na kusema si vizuri viongozi kuwa na mtafaruku wa aina hiyo.

“Tumeshangaa sana wakati tunambiwa kuwa Maangi alipanga maandamano ya kumwaribia Gavana Ongwae jina,” alisema Wilfred Onkoba, mkazi wa Ogembo.