Share news tips with us here at Hivisasa

Naibu Gavana wa Kaunti ya Kisii Joash Maangi amewaomba wakazi wa kaunti hiyo kuungana na kushrikiana na serikali ya kaunti hiyo katika maendeleo.

Maangi alisema ikiwa wakazi wa kaunti hiyo hawatashirikiana na serikali, hakuna maendeleo yatafanywa katika kaunti hiyo.

Akiongea siku ya Alhamisi kwa hafla ya kuzindua ripoti ya utekelezaji wa katiba kwa mara ya pili tangu ipitishwe mwaka wa 2010 katika uwanja wa michezo wa Gusii, Maangi alisema maendeleo mengi yatafikiwa ikiwa kutakuwa na umoja kati ya wakazi na viongozi wote wa kaunti hiyo.

Maangi aliomba viongozi wote wa Kaunti ya Kisii kushirikiana kuleta maendeleo kwa wananchi na kutimiza ahadi walizotoa hapo mbeleni.

Mangi alisema tangu katiba ipitishwe, mengi yamefanywa kwani inatoa uhuru kwa kila mwanchi na viongozi kufanya yale yatanufaisha wananchi.

“Naomba katiba iendelee kutekelezwa jinsi ilivyo kwani katiba imefanya maendeleo kuja mashinani na tutaendelea kuisherekea na kuitumikia kikamilifu hadi tuone tutakapofika kama wananchi wa Kenya,”alisema Maangi.

Matamshi yake ya katiba kuendelea kutekelezwa yaliungwa mkono na Naibu Gavana wa kaunti ya Nyamira Amos Nyaribo na Naibu Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Daniel Kiprotich ambao walisema katiba iendelee kutekelezwa hadi asilimia 100 haswa katika serikali za ugatuzi.