Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Zaidi ya familia elfu nne zimevamiwa na kunguni mjini Nakuru katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.

Hayo ni kulingana na afisa wa afya ya umma katika jimbo la Nakuru Samuel King’ori.

Akiongea na vyombo vya habari mjini Nakuru Jumanne, King’ori alisema kuwa mitaa ya Shabab, Kwa Rhonda na Shabab viungani mwa mji wa Nakuru ni miongoni mwa mitaa iliyoadhirika zaidi.

Amesema kunguni hao pia wamevaamia baadhi ya shule na vituo vya kuwaokoa watoto vilivyoko mjini Nakuru.

Hata hivyo, alidokeza kuwa serikali ya jimbo imeandaa mikakati ya kupiga dawa katika maeneo yaliyoathirika, japo alihofia kwamba mavaamizi hayo ya kunguni yametokana na hulka ya wananchi wengi kuishi katika chumba kimoja, na wengine kutozingatia usafi.

King’ori alidokeza kuwa jumla ya vyumba 1,000 tayari vimepigwa dawa katika maeneo ya Kaptembwo na Shabab huku serikali ya jimbo ikipania kutumia shilingi 20,000 wakati wa zoezi hilo.

Kwa sasa King’ori amewahimiza wananchi kuchukua tahadhari ya mapema katika kuimarisha usafi ili kuzuia kusambaa kwa wadudu hao hatari.