Mhakama kuu mjini Naivasha mapema hii leo imepinga hatua ya mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini (KRA) ya kutaka kupiga marufuku leseni ya kampuni ya vileo ya Keroche Breweries.
Hii ni baada ya kampuni hio ya Keroche kufika mahakamani kutaka tume hiyo ikomeshwe na mahakama kuhujumu operesheni zake hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa na kuamuliwa
Wiki jana mamlaka hayo yaliiandikia kampuni hiyo kuitaka kusitisha shugli zake kwa ghafla kutokana na kile kilichotajwa kama kuhudumu kinyume na sheria.
Kampuni hiyo imekashifu hatua hiyo ambayao wainaitaja kama kinyume cha sheria na ambayo kwa mujibu wao ni mbinu ya wapinzani wao kuiangamiza kampuni hiyo amabayo imekuwa kileleni ka muda mrefu.
“Hii ilikuwa ni mbinu ya wapinzani wetu kutufilisisha kwa kuleta madai yasiyo ya ukweli na msingi dhidi yetu,” alisema Nicholas Kipchirchir, meneja wa kampuni hiyo.
Aliongeza kwamba lengo hilo ni mojawapo ya mbinu kwa mahasidi hao kupaka tope kampuni hiyo abayo inajulikana mno katika sekta ya vileo.
Kipchirchir pia amewadokezea kidole cha lawama KRA huku akisema kelele zao hazitawatia hofu na kuwazuia kuendelea na biashara yao.
“Haya ni kama mawingu yanayopita na kamwe hayatatuzuia kuendeleza shugli zetu na kuzidi kuwahudumia wakenya kama kawaida,” alisema Kipchirchir.
Aliyasema haya alipokuwa akizungumza na wanachama wa bunge la Jimbo la Muranga waliotembelea kiwanda hicho kilichoko mjini Naivasha.