Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Bomachoge Borabu, Joel Onyancha ameziomba bodi zote zinazosimamia shule zilizoko katika eneo bunge lake kutumia pesa za hazina ya ustawi maeneo bunge vizuri.

Akizungumza siku ya Jumatatu katika shule ya wasichana ya Omobera wakati kamati itakayosimamia shule hiyo ilikuwa inachaguliwa, mbunge huyo aliomba bodi zote za shule mbalimbali kutumia pesa hizo vizuri huku akiomba wanakamati kuorodhesha yale yote watafanya kupitia pesa hizo ili kuzuia kukosekana kwa pesa hizo au kupotea kwa pesa hizo.

“Kila kitu mfanyalo kwa shule zenu mkitumia pesa za CDF muandike chini maana hizi pesa ni za maendeleo na hakuna haja ya pesa hizo kupotea. Naomba mjaribu sana kuzitumia vizuri ili viwango vya elimu kuinuka juu zaidi katika shule zetu,” alisema Onyancha.

Mbunge huyo aliowaomba walimu kutia motisha na kuwafundisha watoto kwa bidii ili waweze kupita katika mitihni ya kitaifa huku akiwaomba wanafunzi kutia bidii kwa masomo ili waje kujisaidia nyakati zijazo.

“Naomba walimu na wanafunzi wafanye kazi yao kikamilifu ili viwango vya elimu viinuke zaidi katika eneo bunge langu na katika Kaunti ya Kisii, kama njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa elimu imeimarika kikamilifu eneo la Kisii,” aliongeza Onyancha.