Share news tips with us here at Hivisasa

Mbunge wa eneo bunge la Borabu, Kaunti ya Nyamira ameahidi kuzinunulia shule za upili katika eneo bunge lake mbasi ya shule kabla ya uchaguzi wa mwaka wa 2017.

Hii ni baada ya kuwaahidi wakazi wa eneo hilo kuwa atafanya maendeleo mengi zaidi kabla ya uchuguzi ujao.

Akizungumza siku ya Jumapili nyumbani mwake, baada ya kurudi kutoka nchi ya umarekani alikoenda kwa majuma mawili, mbunge Ben Momanyi alisema kila shule ya upili itapata gari kupitia pesa za hazina ya ustawi maeneo bunge ili kuinua viwango vya masomo na kurahisisha gharama kwa wazazi wakati wanafunzi wanaenda michezo na hata shughuli za kimasomo katika sehemu mbalimbali.

Mbunge huyo pia aliahidi kuweka umeme katika kila shule ya upili na kutengeneza barabara zote zilioko eneo bunge lake ili kurahisisha uchukuzi katika eneo hilo.

“Nitafanya maendeleo mengi kabla ya uchaguzi ujao. Nitaanza kwa kununulia kila shule mabasi kish nitatengeneza barabara na nitaunganisha umeme kwa shule za upili. Nawaomba muniambia chochote mnachotaka nikifanye, ili tufanye maendeleo pamoja,” alisema Momanyi.

Aliongeza, “Mlinichagua niwafanyie maendeleo na nitayafanya ili muweze kufurahia uongozi wangu.”