Mbunge wa Borabu Ben Momanyi amewaomba wananchi wa eneo bunge lake kuungana naye ili kufanikisha mipango ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye eneo bunge lake.
Akizungumza kule Nyansiongo siku ya Jumatatu, Momanyi aliwasihi wananchi kushauriana naye iwapo wataona kwamba kuna maswala fulani yanayofaa kuafikiwa kwa minajili ya maendeleo.
"Ningependa kuwasihi wananchi wa eneo hili kujisikia huru kushauriana nami wakati wanapoona kwamba kuna maswala flani yanafaa kuafikiwa kwa minajili ya maendeleo ya eneo bunge hili," alisihi Momanyi.
Momanyi aidha alihaidi kumaliza ukarabati wa barabara ya Kijauri-Manga-Raitigo-Nyamecheo na Kijauri mtawalia kuanzia mwezi ujao, huku akihaidi kuweka matuta kwenye barabara ya Keroka-Chepilat kama njia mojawapo ya kupunguza visa vya ajali za mara kwa mara ambavyo vimekuwa vikushuhudiwa eneo hilo.
"Nina mipango ya kumaliza ukarabati wa barabara ya Kijauri-Manga-Raitigo-Nyamecheo na Metamaywa, na hivi karibuni nitaweka mipango ya kuweka matuta kwenye barabara ya Keroka-Chepilat kama njia mojawapo ya kupunguza visa vya ajali za mara kwa mara," alisema Momanyi.
Wakazi wa eneo bunge hilo aidha wamemshukru Momanyi kwa mikakati aliyoiweka ili kuendesha miradi ya maendeleo kwenye eneo bunge hilo, huku wakimwomba kuisihi serikali ya kaunti kuwasambazia maji ya mifereji kwa kuwa eneo hilo hukumbwa na ukosefu wa maji.