Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya amehukumiwa kufungo cha miaka kumi gerezani na mahakama moja ya Mombasa.

Mahakama ilielezwa kuwa mnamo Julai 13, 2015 katika eneo la Portreiz huko Changamwe, mshukiwa, Jamal Ochieng, alipatikana pakiti 12 za heroini yenye thamani sh2,400, misokoto miwili ya bangi yenye thamani ya Sh20 na tembe moja ya Rohypnol yenye thamani ya Sh100.

Ochieng alifikishwa mahakamani Julai 14, 2015 na kukanusha mashitaka hayo.

Akitoa hukumu hiyo siku ya Jumatano, Hakimu Mkuu Diana Mwachache alisema kuwa kifungo hicho kitakuwa funzo kwa mshukiwa huyo na walanguzi wengine.

“Hii itakuwa funzo kwa wengine wanaojihusisha na utumizi na ulanguzi wa dawa za kulevya,” alisema Diana.

Mshatikwa huyo alipewa siku 14 kukata rufaa.