Mzee wa umri wa miaka 70 anayekabiliwa na mashtaka ya ubakaji wa msichana wa miaka 13 ametozwa dhamana ya Sh200,000 katika mahakama ya Mombasa.
Mahakama ilielezwa siku ya Jumatano kuwa mshtakiwa, John Nyaga, anadaiwa kumbaka msichana huyo kati ya tarehe Septemba 28 na Octoba 18, 2015 katika eneo la Shonda, Likoni.
Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wakazi walifanikiwa kumtia mbaroni mshukiwa huyo katika eneo hilo la Shonda.
Nyaga alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Susan Shitub siku ya Jumatatu.
Kesi hiyo itasikizwa tarehe Novemba 25, 2015.