Mwanamume mmoja alifikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru siku ya Jumatano kujibu shtaka la wizi wa vipuri vya gari vyenye thamani ya Sh320,000.
Peter Yegon anadaiwa kuiba vipande vya gari aina ya Mercedes Benz, vyenye thamani ya Sh320,000, katika duka la Biashara Master lililo mjini Njoro, mnamo tarehe Oktoba 20, 2015.
Yegon pia alikabiliwa na shtaka la pili la kupatikana na mali ya wizi katika kituo cha kibiashara cha Maili Tatu Trading Centre, mjini Njoro.
Yegon hata hivyo alikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu mkuu Liz Gicheha na akawachiliwa kwa bondi ya Sh100,000 na mthamini wa kiasi sawia au Sh50,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tarehe Oktoba 11 na kusikizwa tarehe Disemba 29, 2015.