Share news tips with us here at Hivisasa

Mwakilishi mteule katika Kaunti ya Kisii Velstus Metobo amempongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kusimama kidete kukana ndoa ya jisia moja nchini.

Hii ni baada ya Rais Kenyatta kukana ndoa ya jinsia moja mnamo siku ya Jumamosi alipokuwa na Rais wa Marekani Barack Obama katika makao ya ikulu ya rais jijini Nairobi.

Rais Kenyatta alikuwa akihutubia Waandishi wa habari ambapo alisema ndoa kati ya jinsia moja inaenda kinyume na tamaduni ya Kenya ingawa Rais Obama aliyekuwa nchini tangu Ijumaa amekuwa akipigia debe ndoa hiyo ni haki na uamuzi wa mtu kufanya hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa habari siku ya Jumapili katika mji wa Kisii, Mwakilishi Metobo alisema jinsi Uhuru Kenyatta alikana ndoa hiyo ni kuonyesha haki kwa Wakenya kwani katika bibilia hairuhusiwi ndoa aina hiyo kufanyika kamwe na kusema nchi zile ambazo zinakubali hayo kibibilia ni ukiukaji au ni kinyume.

“Namshukuru Rais Kenyataa kwa kusema ndoa hiyo haiwezi kubaliwa katika nchi ya Kenya. Mungu alimuumba mume waoane na mke bali sio mke kwa mwanamke mwingine au mume kwa mwanamume mwingine,” alisema Metobo, Mwakilishi mteule katika Kaunti ya Kisii.

Wakati uo huo, mwakilishi huyo aliwaomba wazazi katika kaunti hiyo kuwapa wanao mafunzo ya kuwajenga kimaisha na kuwasomesha ili nao waje kujisaidia nyakati zijazo.

"Wazazi wote nawaomba mfundishe watoto wenu tabia iliyo nzuri ambayo itawajenga kimaisha na kuwa wenye nidhamu katika jamii,” aliongeza Metobo.