Mwanajeshi mmoja anayedaiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 20 alifikishwa mbele ya mahakama ya Nakuru siku ya Jumatatu kujibu shtaka hilo.
Evans Ochieng Akello, ambaye ni afisa mwenye ngazi ya kanali anadaiwa kutekeleza kitendo hicho tarehe Oktoba 22, 2015 katika eneo la Lanet viungani mwa mji wa Nakuru.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo mbele ya Hakimu Mkuu Liz Gicheha, huku akijitetea kuwa walijiburudisha kwa kutumia vileo na mlalamishi siku hiyo, na baadaye walikubaliana kula uroda.
Mshtakiwa huyo aliachiliwa kwa bondi ya Sh200,000 au Sh100,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa tarehe Novemba 12, 2015 na kusikizwa tarehe Disemba 10, 2015.