Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamke wa umri wa makamo amefikishwa mahakamani kwa shtaka la kujaribu kumuua mtoto wa miaka mitano kwa kumpa sumu.

Mwendesha mashtaka katika mahakama ya Mombasa Lydia Kagori aliiambia mahakama siku ya Jumatatu kuwa mnamo tarehe 14 Oktoba, mshukiwa huyo anadaiwa kumpa sumu mtoto huyo mvulana katika eneo la Changamwe.

Mshtakiwa aliiambia mahakama kuwa mshukiwa alitiwa mbaroni punde tu baada ya mtoto huyo kugonjeka na kufikishwa hospitalini baada ya kunywesha sumu.

Mshtakiwa alikanusha mashtaka hayo mbele ya hakimu wa Mombasa Susan Shitub, na aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja, huku kesi yake ikitarajiwa kusikizwa mnamo tarehe 23 mwezi Novemba mwaka huu.