Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanamume alifikishwa mbele ya mahakama moja ya Nakuru kwa shtaka la jaribio la unajisi.

Kiongozi la shtaka aliambia korti kwamba mnamo tarehe 22 mwezi Juni mshukiwa kwa jina Julius Mukii alijaribu kumbaka msichana mmoja mwenye umri wa miaka 11 katika eneo la Rongai katika Jimbo la Nakuru.

Mshukiwa Mukii ilisemekana alimteka msichana huyo akitoka shuleni na kumvuta kwenye kichaka kilichoko kando ya barabara ambapo alijaribu kumpapasa katika sehemu zake za siri kisha kujaribu kumnajisi kabla ya mshichana huyo kupiga mayowe na kuokolewa na wapita njia huku mshukiwa huyo akitoweka.

Korti iliambiwa kuwa mshukiwa huyo alikamatwa na maafisa wa Kituo cha Polisi cha Central ya Nakuru siku chache baadaye na kufikishwa katika kituo cha polisi na kisha mahakamani kujibu mashtaka hayo.

Akijitetea mbele ya mahakama, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo huku akisema kuwa sio ya kweli na hayana msingi wowote.

Hakimu katika mahakama hiyo Doreen Mulekyo alisema visa vya unajisi wa watoto vimeongezeka sana katika eneo la Nakuru huku akisema kuwa ni dhulma kubwa kwa watoto hao wenye umri mdogo.

Mshukiwa atazidi kuzuiliwa korokoroni hadi kesi hiyo itakaposikizwa tena tarehe 27 mwezi Julai mwaka huu.