Mwanaume mmoja alifikishwa mbele ya mahakama moja ya Nakuru mapema siku ya Jumatano kujibu shtaka la mauaji.
Mshukiwa huyo kwa jina David Kosgei anakisiwa kumuua babake shadrack Kosgei mnamo Novemba 6, 2011 muda wa saa nane mchana katika kijiji cha Sigoro, Eldama Ravine katika eneo la bonde la ufa.
Mshukiwa Kosgei anadaiwa kusababisha kifo cha babake kwa kumpiga kwa mbao kwa madai kuwa babake alikuwa anatishia kumuua kama alivyo muua mwanawe mwingiene hapo awali kutokana na ugomvi wa kinyumbani.
Korti iliambiwa kuwa kakake mdogo mshukiwa Christopher Kosgei alikuwepo na kusuhudia kisa hicho aliripoti kisa hicho kwenye Kituo cha Polisi cha Eldama Ravine ambako mshukiwa alishikwa na kuzuiliwa.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkuu Doreen Mulekyo, Shahidi Christopher alieleza korti kilichotokea siku hiyo.
“Kakangu mkubwa alirejea nyumbani muda wa saa nane mchana na kuanza kugombana na marehemu babangu kabla ya kuchukua mbao iliyokuwepo karibu na kumgonga kichwani na kumuua papo hapo,” alisema shahidi Christopher.
Akijitetea mbele ya mahakama hiyo, mshukiwa alikana mashtaka hayo na kusema kuwa walikuwa wakiongea na babake kabla ya marehemu kuanguka na kuzimia papo hapo.
Kesi hiyo itasikizwa tena mwezi Oktoba 13, mwaka huu.