Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Licha ya mengi kusemwa kuhusu 'kusoma katiba' ya wenzio, mwanaume mmoja siku ya Ijumaa mwendo wa saa kumi mchana alipatikana kwa pupa akiwa anakula uroda na mke wa mtu mjini Kisii.

Katika chumba cha wageni al maarufu Guest House cha MIDTOWN, mwanamke mmoja alifumaniwa na mumewe wa miaka saba sasa katika ndoa katika chuma cha wageni hicho akiwa na mwanamume mwingine wakionana kimwili.

Kisa hicho kilitatiza hali ya biashara mjini humo hadi wenye maduka kufunga kwa hofu ya kuvamiwa na umati uliojawa na gadhabu nyingi mno.

Bwana huyo alidai kuwa amekua akisikia fununu kuwa mkewe, ambaye wamepata naye watoto wawili tayari amekua akishirika mapenzi na jamaa huyo ambaye alitoka mguu niponye bila nguo akimwacha mwanamke huyo mikononi mwa wananchi.

Aidha, alisema alipata simu kutoka kwa rafikiye ambaye alimelekeza waliokuwa 'wakikagua miradhi'. Mama huyo ilisemekana ana duka la kuuza maji mjini Kisii huku mumewe akiwa mchuuzi wa bidhaa humo mjini.

Mwanamke huyo alikana madai hayo akisema ni leo tu walienda katika chumba hicho na hajawahi fanya kitendo kama hicho tangu aoleka na mumewe.

Wanawake waliojawa na hasira kwa kuchafuliwa jina kama wamama kwa kitendo hicho cha mama huyo, walimpa adhabu na kumwelekeza maeneo ya nyanchwa anakopangisha wakidai watamwamisha mjini Kisii.

"… hii ni aibu ilioje mke na mama wa watoto wawili mchana huu wote anaacha biashara yake kuenda kukula uroda na mume ambaye hata siye mumewe? Tutamsindikiza hadi anakokodisha nyumba na kumpeleka kwao eneno la Magomb, Kaunti ya Nyamira sasa hivi...," alisema mama Eunice Eriki kwa hamaki.

Aidha aliwaonya akina mama wa tabia kama hiyo kukoma na kusema kuwa hawataki aibu ndogo ndogo kama hiyo ya kuwachafulia wakina mama jina mjini Kisii.