Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 30 alipatikana ameuawa nyumbani mwake katika eneo la Chebilat, Kaunti ya Nyamira.
Duke Momanyi, ambaye ni mwanabiashara katika eneo la Chebilat alipatikana hii leo, Jumatatu ameuawa kwa kukatwakatwa.
Akithibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi Wilayani Borabu Athony Onyango alisema huenda ikawa mwendazake aliuawa katika eneo tofauti na kisha kuletwa kwake kwani wakaazi ambao wako karibu na marehemu hawakusikia chochote kuhusu mauaji hayo wakati wa usiku.
“Naomba wananchi wote kuanzia leo wasifike kwa mauaji yoyote kwa sababu wakaazi hao huaribu ushahidi haswa uchungunzi unapoanzishwa,” alisema Athony Onyango, mkuu wa polisi wilayani Borabu.
Aidha, wakaazi wa eneo hilo wamewaomba maafisa wa usalama kuingilia kati kuchunguza mauaji ambayo yamekuwa yakiongezeaka katika eneo hilo kila wakati.
“Katika eneo hili letu la Chebilat watu wamekuwa wakiuawa sana, tunaomba maafisa wa polisi kufanya uchungunzi kwa kina,” alihoji Mary Morara, mkaazi.
Kwa sasa, maafisa wa polisi wa kituo cha Chebilat wameanzisha uchungunzi kuhusiana na mauaji hayo ya mwanamume huyo.