Share news tips with us here at Hivisasa

Mhudumu mmoja katika eneo la Ondiri ametiwa mbaroni na maafisa wa polisi kwa madai ya kuuza filamu za ngono.

Mshukiwa huyo anadaiwa kuwauzia watoto wa shule filamu hizo kwa muda wa miaka miwili sasa. Wakazi wa eneo hilo walimfumania na kuwaita maafisa wa usalama ili kumtia mshukiwa mbaroni.

Akizungumza siku ya Ijumaa wakati wa tukio hilo, mkazi wa eneo hilo Rose Kimindi alidai kwamba mhudumu huyo amekuwa akiwauzia watu filamu hizo hasusan watoto kwa muda mrefu.

Kimindi alisema kuwa alimpata mtoto wake akitazama filamu hiyo alipokuwa aliporejea kutoka kazini.

Alieleza kuwa baada ya kuiharibu na kumwadhibu mtoto wake, alifichua kuwa mhudumu huyo ndiye aliyemuuzia filamu hiyo.

Alisema kuwa hiyo haikuwa tukio la kwanza kwa kuwa wazazi wengine walilalamikia jambo hilo lakini mshukiwa alikana shtaka hilo.

"Filamu hizi zimepotosha watoto wetu na leo tumeamua kwamba tunataka sheria ichukuliwe dhidi ya mshikiwa," alisema Kimindi.

Akidhibitisha kisa hicho, mkuu wa polisi katika eneo la Kikuyu Mutune Maweu aliwapongeza wakazi kwa kuchukua hatua ya kuwafahamisha polisi badala ya kuchukua sheria mikononi mwao.

Alisema kwamba polisi walimtia mbaroni mshukiwa huyo na waliweza kunasa filamu 65 za ngono wakati wa kumshika mshukiwa katika duka lake la kuuza filamu hizo.

"Uchunguzi unaendelea na tunawahakikishia wakazi kwamba haki itatendeka.Hata hivyo, hii ni onyo kwa wale wanaouza filamu wajue ni hatia kuuza filamu za ngono kwa kuwa zinapotosha jamii," alisema Maweu.