Share news tips with us here at Hivisasa

Mwanasiasa kutoka eneo Bunge la Nyaribari Chache Ben Mogaka ameahidi kutoa msaada wa tarakilishi 10 kwa shule ya upili ya wavulana ya Amasago kama njia moja ya kuinua viwango vya elimu.

Akiongea siku ya Alhamisi katika shule hiyo ilioko eneo la Keumbu, Kaunti ya Kisii katika hafla ya kutoa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vyema katika mtihani wa kitaifa wa mwaka jana, Mwanasiasa huyo ambaye ana azma ya kuwania kiti cha ubunge katika eneo bunge hilo aliota taraklishi kumi kama njia moja ya kusaidia shule hiyo kujiendeleza kimasomo.

"Nimetoa tarakilishi 10 ili kusaidia masomo katika shule hii kama tuzo baada ya kufanya vyema katika mtihani wa mwaka jana. Ninawaahidi kuwa nitakuwa nakifanya hivyo kila mwaka ilkiwa wataendelea kufanya vyema zaidi kwa kuzoa alama ya juu zaidi kwenye mtihani wa mwaka huu," alihoji Mogaka.

Kwingineko, Mogaka alisema kuwa ameanzisha mradi wa kupeana chakula kwa baadhi ya shule ili kusaidia wanafunzi na chakula huku akiahidi gunia tatu za mahindi na moja ya mharagwe kwa shule ya Amasago kama njia moja ya kujali maslahi ya wanafunzi hao.

Aidha, mwanasiasa huyo aliwaomba viongozi wote walioko uongozini na wanao azma ya kuwania viti mbali mbali kushirikiana ili kuinua viwango vya maendeleo na masomo katika Kaunti ya Kisii.

Kwa mujibu wa mwanasiasa huyo, kutokana na usaidizi wa chakula katika shule, viwango vya elimu vimeimarika na kuapa kuendelea kusaidia shule zingine katika eneo Bunge la Nyaribari Chache.