Wakazi wa mtaa wa Mwembe wanaofanya kazi ya Jua Kali wamewaomba maafisa wa polisi kuwasaka wanaowaibia vyuma vya kutengenezea vifaa mbali mbali.
Wakiongea siku ya Ijumaa na Mwaandishi huyu katika mtaa huo iliyoko katika Wadi ya Kisii ya Kati, eneo bunge la Nyaribari Chache katika Kaunti ya Kisii, wafanyikazi hao walisema wanaghadhabishwa na baadhi ya watu wanaowaibia chuma hizo wanazotumia kutengenezea vifaa mbalimbali kama dirisha, milango miongoni mwa vitu vingine.
Kwa sasa wamewaomba maafisa hao kuwasaka watu hao na kuwachukulia hatua kwani wamekuwa na mazoea ya kuwaibia kila wakati, jambo ambalo wanakerwa nalo kwa kupata hasara kubwa.
“Nawomba maafisa wetu wa polisi kuwasaka watu hao kwa kuwa wametuhangaisha na kutupeleka hasara kubwa katika sekta hii,” alihoji Davidson Mogere,mfanyikazi wa Jua Kali.
Wafanyikazi hao wamewaonya wanaofanya kazi ya kukushanya vifaa vya chuma katika mtaa huo kwa kusema huenda wakachangia vyuma vyao kupotea huku wakisema kuwa yeyote atakayepatikana na chuma katika mtaa huo atachukuliwa hatua kali ya kisheria.
“Kuna baadhi ya watu wanaokushanya vifaa vya vyuma ili kuenda kuviuza ili kupata pesa. Kwa sasa wawe wakijua kuwa siku zao zinahesabiwa,” alidokeza Charles Matangi, mfanyibiashara.
Aidha, wakazi wa mtaa huo wa Mwembe wameombwa kushirikiana na polisi na wafanyibiashara hao kwa kutoa ripoti ya mshukiwa yeyote ili sheria kuchukua mkondo wake.