Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Maafisa wa polisi waliojukumika kuhifadhi dawa za kulevya aina ya bangi iliyonaswa kutoka kwa washukiwa mwaka jana walisababisha kicheko baada ya kudai kuwa bangi walioweka kwenye hifadhi ya polisi iliweza kuliwa na panya.

Maafisa hao ambao walikuwa wakitoa ushahidi siku ya Ijumaa katika mahakama ya Kwale dhidi kesi ya washukiwa wanne ambao walishtakiwa kwa kuwa na misokoto ya bangi 540, walizua kioja kwa kudai kuwa misokoto hiyo haikuwa mahali walihifadhi na huenda ilililiwa na panya.

Mafisa hao walikuwa wakitoa ushahidi katika mahakama ya Kwale dhidi ya washukiwa wanne ambao walinaswa katika eneo la Banga kanda ya Pwani Kusini, ambapo walikuwa wanasafirisha dawa hizo za kulevya za aina ya bangi kutoka kaunti ya Migori, na walikuwa na zaidi ya vifurushi elfu moja mia saba.

Maafisa hao walieliezea mahakama mbele ya hakimu mkaazi Paul Mutai na kudai kuwa idadi ya misokoto ambayo walikuwa wamehifadhi katika eneo la kuwekea vitu vya ushahidi katika kituo cha polisi cha matuga ilikuwa imepungua na huenda ililiwa na mnyama aina ya panya ambao huwa kwenye hifadhi hiyo.

Hata hivyo kesi hiyo inaendelea kusikilizwa na itaendelea baada ya miezi miwili, mnamo tarehe 16 mwezi wa kumi na mbili mwaka huu.