Seneta wa kaunti ya Nyamira Kennedy Okong’o ameahidi kushirikiana na washikadau wa shule zilizoko Nyamira kuinua viwango vya elimu.
Akiongea siku ya Jumapili katika shule ya msingi ya Gesure alipotembelea shule 10 za msingi katika eneo bunge la Mugirango Kaskazini, senator Okong’o alisema maswala ya elimu ni muhimu sana katika jammi na yanafaa kuyainuliwa kwa viwango vya juu.
Baadhi ya shule za msingi alizozitembelea ni Misambi, Gesure, Nyamusi, Nyakemina, Ntaana, Kiomachingi, Getonto na Nyabiore huku akizipa shule hizo vitabu vya kusoma vilivyogharimu Sh300,000 na miti 5,000 za kupandwa katika shule hizo kama njia moja ya kuimarisha mazingira katika Kaunti ya Nyamira.
Wakati uo huo, seneta Okong’o aliwalipa mshahara walimu watano wa shule ya Gesure kwa mwezi mmoja haswa wale wameajiriwa na wazazi.
Okong’o pia aliwaomba wazazi, walimu, viongionzi na wanafunzi kujiunga pamoja kuona kuwa viwango vya elimu vimeinuliwa zaidi katika kaunti nzima ya Nyamira.
“Ningependa kila upande, iwe ni upande wa walimu, viongonzi na wazazi kushirikiana na wanafunzi ili watueleze ni nini hawana, kile kimekosa katika shule zao ili tukishughulikie, na hivyo elimu itakuwa ya kufurahisha sana katika kaunti yetu ya Nyamira,” alisema Kennedy Okong’o, seneta wa Kaunti ya Nyamira.