Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mshauri mkuu wa Benki ya Dunia Charles Mochama amekosoa serikali ya kaunti ya Nyamira kwa kutowateua vijana katika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya kaunti hiyo.

Kulingana na mshauri huyo, nyadhifa nyingi za serikali ya kaunti hiyo zimemilikiwa na watu ambao wamewai tumikia nyadhifa mbalimbali za serikali hapo awali, na kusema kuna haja ya serikali ya kaunti hiyo kuwa na uwazi wakati nafasi za ajira zinapotolewa kwa wafanyikazi wa umma.

Akizungumza mnamo siku ya Jumanne katika mji wa Nyamira, Mochama alisema ni picha mbaya serikali ya kaunti huonyesha kwa wapiga kuwa wakati hawaonyeshi uwazi kwa kila mwananchi wa kaunti hiyo.

Wakati huo huo, Mochama aliomba wananchi wa kaunti ya Nyamira kumchagua katika uchaguzi ujao kuwa gavana wa kaunti hiyo ili kuleta maendeleo zaidi, na kuwapa ajira wananchi wa kila aina kati yao vijana na watu wazima ili kuona kuwa kumekuwa na uwazi kwa pande zote mbili bila kutenga yeyote.

“Si vizuri vijana wetu wa umri mdogo wenye elimu kutoteuliwa katika nyadhifa za serikali ya kaunti yetu,” alisema Mochama.

Aidha, afisa huyo amewaomba vijana wote wa kaunti hiyo kutafuta mbinu ya kujiendeleza kwa kuanzisha vikundi vya biashara ili kufaidika katika siku zijazo na kupunguza hali ya umasikini miongoni mwao.