Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi kutoka eneo bunge la Kitutu Chache kusini kaunti ya Kisii wamewalaumu viongonzi wa Kisii kwa kutoshirikiana pamoja ili kuleta maendeleo.

Hii ni baada ya wakaazi hao kulalamikia barabara mbovu ya kutoka eneo la Nyamataro kuelekea mji mkuu wa Kisii.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumapili, wakazi hao wakiongozwa na victor Ogeto walisema barabara hiyo imekuwa mbaya na haipitiki kamwe na kumwomba mbunge wa eneo bunge hilo la Kitutu Chache Kusini, Richard Momoima Onyonka kushirikiana na Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ili waweze kukarabati barabara hiyo.

Haya yanajiri siku chache baada ya waendeshaji bodaboda wa eneo hilo kuandamana na kupanda migomba katika barabara hiyo, jambo ambalo wameapa kuwa hawatawacha mpaka hatua ichukuliwe na barabara kutengenezwa.

“Tunataka barabara hii itengenezwa haraka kwasababu wananchi wa eneo hili wanasumbuka sana hasa wakati mvua inaponyesha. Hatua ya kukarabati barabara hii ichukuliwe haraka kwani viongonzi walichaguliwa kufanya maendeleo,” alisema Daniel Obino, mkazi wa eneo hilo.

Aidha, wakazi hao walisema wanasumbuka sana kwani wanalazimika kutumia kutumia njia mbadala ambayo ni ndefu.

Tunaomba wahusika ambao ni viongonzi waonyeshe uwazi na huruma kwa wananchi wa eneo hili kwa kukarabati barabara hili ambalo kwa sasa ni hatari kwa maisha ya watu ambao wanaitumia,” alisema Nemiah Mokaya, mkazi wa eneo hilo.