Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakazi kutoka eneo la Nyangweta, eneo bunge la Mugirango kusini kaunti ya Kisii wameomba serikali kuwahakikishia usalama wao kikamilifu.

Hii ni baada ya usalama kudorora zaidi katika eneo hilo, huku visa vingi vya uhalifu vikiripotiwa, ikizingatiwa wiki jana mwanamke mmoja alishambuliwa na kuawa katika eneo hilo, jambo ambalo limeua taharuki kubwa miongoni mwa wakaazi hao.

Wakizungumza na waandishi wa habari siku ya Jumamosi katika eneo hilo la Nyangweta, wakaazi wa eneo hilo waliokuwa na hasira nyingi wakiongozwa na Davidson Nyatuka walisihi na kuomba serikali kuwahakikishia usalama wao, kwani wameogopa kuwa huenda watu wengi waendelee kupoteza maisha yao wanapotumia barabra za eneo hilo.

“Kwa nini sehemu zingine usalama huwa unaimarishwa baada ya wakaazi kuitisha usaidizi huo? Kuna majambazi ambao wanaendelea kuwashambulia watu wetu kila wakati, tunaomba serikali yetu kutuhakikishia usalama maana sisi sote ni wakenya,” alihoji Godfrey Makworo, mkaazi wa eneo hilo.

Wakaazi hao wamekuwa wakilia serikali kuwahakikishia usalama wao, lakini hadi sasa hakuna hatua imechukuliwa kuwasaidia.

Wakazi hao sasa wanaomba serikali kuruhusu maafisa wa vitengo mbalimba wa polisi kushika doria katika eneo hilo mchana na usiku, ili kupunguza visa vya wakazi kushambuliwa kila mara.

“Sisi tuko na subira ili serikali itukumbuke kwa kutuhakishia usalama wetu,” alisema Vellah Kenyaya, mkazi mwingine.