Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa bodaboda na magari katika mji wa Kisii wameiomba serikali ya Kaunti ya Kisii kukarabati barabara ya Daraja Moja kuingia mjini inayounganisha barabara kutoka Keroka, Nyamira na Kiligoris. 

Wakiongea siku ya Jumatatu katika barabara hiyo ilioko karibu na hospitali ya kibnafsi ya Ram mjini Kisii, walisema kuwa ajali nyingi husababishwa na mashimo ambayo yamekuwa kwa muda katika barabara hiyo. 

“Tunaomba serikali ya kaunti yua Kisii kuingilia kati na kukarabati barabara hii ili kutusaidia sisi kama wahudumu katika sekta ya uchukuzi," alsiema Davidson Mireri, mwendeshaji bodaboda.

Kwingineko, walitaka kujua kama barabara hiyo inastahili kukarabatiwa na serikali kuu kwani kulingana na ripoti walizopata kutoka serikali ya Kaunti ni kuwa kuna barabara zinazostaili kukarabatiwa na serikali kuu na baadhi ya kukarabatiwa na seriklai ya kaunti.  

“Sisi tunaomba barabara hii ikarabatiwe na serikali kuu au serikali ya kaunti. Tunaomba anayehusika  atusaidie kwani tunaendelea kuumia kila siku,” alisema Hezron Nyabiemba, mkaazi.

Wahudumu hao waliomba serikali kuwaruhusu kupitia barabara zingine iwapo ukarabati hautafanywa.