Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya wakazi wa Kisii wameiomba serikali ya Kaunti ya Kisii kutatua mizozo za kila mara katika kaunti hiyo kuhusu kutolipwa kwa wafanyikazi na wanakandarasi baada ya kutoa huduma yao.

Wakiongea siku ya Jumatatu katika mji wa Kisii, baadhi ya wakazi waliongea na Waandishi wa habari walisema migogoro na maandamano zinazoshuhudiwa katika kaunti hiyo huenda zikarudisha maendeleo nyuma, jambo ambalo walisema linastahili kutatuliwa mapema kabla ya kumea mizizi katika kaunti hiyo.

Kwa sasa wameiomba wanaohusika na malipo katika serikali hiyo ikiongozwa na Gavana James Ongwea kutafuta suluhu la mapema kwani migogoro hiyo husababisha uchumi na maendeleo kukwama.

“Serikali ya kaunti yetu inastahili kushughulikia masuala kama haya haraka ili mizozo kama hizi zisiwe zikishuhudiwa kila mara kwani ni aibu watu kugoma kila wakati kwa ajili ya kutolipwa mishahara yao,” alihoji Albert Osoro mkazi.

Haya yanajiri baada ya kandarasi waliopewa kazi katika kaunti hiyo kufika katika ofisi za gavana Ongwae siku ya Jumatatu kulalamikia kutolipwa misahara yao, jambo ambalo limewakera wakazi wengi na kusema serikali ya kaunti inastahili kuwajibika na kuwalipa watu hao pesa zao kama anjia moja ya kuzuia maandamano ya kila wakati katika Kaunti ya Kisii.

Aidha, wakazi hao walisema kuna umuhimu wa kutafuta njia mwafaka ya kutatua shida kama hizo licha ya watu kuandamana.

“Naomba serikali yetu kutafuta njia mbadala ya kutatua shida kama hizi kama njia moja ya kuleta uhushianbo mwema kati yake na wafanyikazi, wanaopewa kandarasi ya kufanya kazi katika kaunti hii,” alihoji Reuben Mosige, mkazi.