Mkurungezi wa Mashtaka ya umma nchini Keriako Tobiko amefutilia mbali kesi iliyokuwa inamkabili Gavana wa Mombasa Hassan Joho kwa madai ya ufisadi.
Katika taarifa yake aliyotoa Jumatano, Tobiko alielezea kuwa kesi hiyo ilikosa ushahidi wa kutosha kumpata Joho na hatia, na hivyo hakuwa na budi kuifunga.
Joho alikuwa miongoni mwa maafisa wa serikali waliotajwa kuhusika na ufisadi na Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini (EACC) kwenye orodha iliyokabidhiwa rais Uhuru Kenyatta.
Joho alidaiwa kuhusika na uuzaji wa soko la Mwembetayari iliyoko mjini Mombasa kwa mmliki mmoja wa kibinafsi.
Gavana huyo hata hivyo alikana madai hayo na kusema kuwa uuzaji huo ulifanyika kabla ya kuchukua uongozi wa kaunti hiyo.
Hata hivyo Joho sasa yuko huru kutokana na madai hayo.