Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Chache, Richard Tong’i ameanzisha ujenzi wa chuo cha ufundi katika eneo la Masongo ili vijana kupata fursa ya kusomea taaluma mbalimbali za kiufundi.

Akizungumza siku ya Jumatano katika eneo la Masongo, Tongi aliwaomba vijana ambao hawakupata fursa ya kujiunga na vyuo nchini kujiunga katika vyuo vya ufundi ili kusomea taaluma za kiufundi na kujiimarisha na kujiendeleza kupitia taaluma watakazo zisomea.

Tong'i alisema kuwa nchi ya Kenya inahitaji watu ambao wamesomea taaluma mbalimbali jambo ambalo lilimfanya kuanzisha taasisi hiyo ya kiufundi katika eneo la Masongo ili vijana wapate elimu itakayo wasaidia siku za usoni.

Mbunge huyo alisema kuwa masomo ni ya muhimu kwa binadamu huku akiwaomba vijana kutia motisha katika masomo kama njia moja ya kutengeneza maisha ya kesho.

“Nawaomba vijana ambao hawakujiunga na chuo chochote kufuatia ukosefu wa pesa, kutopita mtihani wa kitaifa vizuri na sababu zingininezo, wajiunge na chuo hiki cha ufundi ili mupate nafasi ya kusomea taaluma mbalimbali,” alisema Tong'i.

Tong’i pia alizuru miradi ya maendeleo katika eneo bunge lake ambayo hufanywa kupitia hazina ya ustawi maeneo bunge, huku akitembelea shule ya upili ya Kerera ambapo ujenzi wa maktaba ya vitabu unaendelea.