Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Miezi mitatu baada ya steji mpya ya magari ya kutoka na kuingia katika mji wa Kisii kufunguliwa rasmi, awamu ya pili ya kukarabati steji hiyo itaanza hivi karibuni.

Steji hiyo ambayo iko nyuma ya duka kuu la Tuskys inahudumia magari ambayo huelekea maneo ya Keroka, Mwembe, Nyamira pamoja na mitaa mingine ambayo hufikiwa kwa kutumia magari ya kukodi ya teksi.

Kulingana na waziri wa mipangilio ya miji na ardhi ambaye alizungumza na mwandishi huyu katika afisi yake siku ya Jumatano Bwana Moses Onderi, kituo hicho cha magari kitaboreshwa na kulainishwa katika robo ya kwanza ya bajeti ya mwaka wa 2015/16, na kuwataka wahudumu wote wa magari katika kituo hicho pamoja na abiria kuwa na subira huku wizara yake ikilishughulikia.

Onderi pia alisema kuwa kuna mikakati mahusus ya kuimarisha viwango vya usafi katika vituo vyote na masoko yaliyoko katika kaunti ya Kisii, na kuwataka wakazi, hasa wafanyabiashara ambao ndio wahusika wakuu kusaidia kufanikisha miradi hiyo.

Vile vile,Onderi aliwaomba kina mama ambao wanaofanya shugli za biashara kando ya steji hiyo kuhakikisha kuwa kuna usafi, wanapotekeleza shughuli za kuuza mboga na matunda yao.