Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana katika eneo la Kinoo wamehimizwa kuhudhuria mafunzo ya kibiashara yaliyopangwa na idara ya vijana yatakayo anza siku ya Jumamosi.

Akizungumza katika ofisi yake siku ya Ijumaa, naibu afisa wa idara ya vijana katika eneo la Kikuyu Bi Violet Nzioki, alisema kwamba mafuzo hayo yalitengewa vijana wa Kinoo ili kuweza kuwanufaisha kibiashara.

Alisema kusudi lao ilikuwa kuhakikisha vijana wanahekima inayofaa ili kuweza kuanza biashara zao.

Nzioki alisema hapo awali vijana hawakujitokeza kwa wingi jinsi ilitarajiwa, hivyo basi kutonufaisha vijana wengi walivyotarajia.

Alisema kwamba mafunzo haya yana umuhimu sana kwa vijana kwa kuwa wao ndio wanaoweza kubadilisha uchumi wa nchi.

Alisema ofisi yao inawapa mikopo vijana pindi tu wanapotaka mikopo ya kuanzisha biashara, na kusisitiza kwamba mikopo hiyo inapewa vijana ambao wamejiunga na makundi mbalimbali na kusajili makundi hayo.

"Ni vyema vijana wakitokeza kwa wingi kwa kuwa mafunzo haya yametengewa vijana. Mafunzo haya ni ya bure na ya manufaa makubwa sana kwa vijana wote ndiposa nawahimiza wajitokeze ili waweze kunufaika," alisema Nzioki.

Nzioki alisema vijana wasimpe yeyote pesa kwa kuwa mafunzo hayo yanatolewa bila malipo.

Alisema hapo awali kuna walaghai ambao walikuwa wamekuja na mbinu ya kuwalaghai watu kwa kuwalipisha wananchi kwa mafunzo ya aina hii.

Nzioki aliwasihii vijana wasinaswe kwa mitego ya aina hiyo akisema kwamba swala hilo litashughulikiwa kuhakikisha hakuna yeyote atalaghaiwa.