Mawaziri, wawakilishi wa wadi, na maafisa wengine wa serikali katika Kaunti ya Nyamira wameombwa kushirikiana pamoja kuhakikisha maendeleo yamefanywa kikamilifu.
Wito huo ulitolewa na katibu wa Kaunti ya Nyamira Erick Aori, ambaye alisema kuwa umoja utaleta maendeleo kwa wananchi wa Kaunti ya Nyamira.
Akizungumza siku ya Jumatatu katika mkahawa mmoja mjini Kisii, wakati wawawakilishi wa wadi, mawaziri na maafisa wengine wa serikali ya Kaunti ya Nyamira walikuwa na mkutano wa kupanga miradi ambayo watafanya, Aori aliowaomba kushirikiana ili kuleta matunda ya maendeleo kwa wananchi.
“Naomba mawaziri, maafisa wa serikali na wawakilishi wote wa serikali ya kaunti yetu ya Nyamira kuwa na umoja ili tuafike maendeleo,” alisema Aori.
Serikali ya Kaunti ya Nyamira imekuwa ikikosolewa na wananchi wa kaunti hiyo kwa kutofanya maendeleo jinsi inavyohitajika.
Baadhi ya miradi viongozi hao walipanga kufanya ni ya kukarabati barabara, kuweka maji na maendeleo mengine ili kaunti ya Nyamira iliweze kuinuka kimaendeleo.