Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa Kaunti ya Nakuru wamekashifu waanadlizi wa maonyesho ya kilimo ya Nakuru yaliyokamilika juzi kutokana na kutozingatia usafi wa vyoo.

Wakiongea na Waandishi wa habari, wakazi hao walidokeza kwamba vyoo hivyo vilikuwa vichafu kupindukia na havikutengewa watu wa kuvitunza. Waliongeza kawamba vilikuwa vimejaa chango na harufu isiyopendeza.

“Havikuwa vimesafishwa tangu maonyesho ya kilimo ya mwaka uliopita na harufu ilikuwa ikitokea kwa umbali. Cha kushangaza ni kwamba hivyo ndivyo vyoo pekee vilivyokuwepo katika uwanja huo,” alidai Nyawira ambaye ni mkazi wa eneo hilo.

Aliongeza kwamba vyoo hivyo vilikuwa vimeundwa kutumia mabati ambayo yalikuwa yamedhoofika sana ikilinganishwa na maeneo mengine kwenye maonyesho hayo ambayo yalikuwa yamepambwa kweli kweli.

Kwa mujibu wa Lenny Gakobo ambaye alihudhuria maonyesho hayo, hio ilikuwa ni picha mbaya mno haswa kwa kuwa maonyesho hayo ya kilimo yalivutia watu wengi mno kutoka sehemu mbali mbali.

Aliongeza kwamba walilazimika kuwaruhusu wanao kivitumia vyoo hivyo kwani hawakuwa na namna nyngine huku akihofia kuwa huenda wakapatikana na maradhi kama ya kipindupindu.

Wameiomba serikali ya Kaunti ya Nakuru ikiongozwa na Gavana Kinuthia Mbugua kushughulikia suala hilo kwa haraka ili kutoleta aibu kama hizo tena.

Afisa wa afya katika eneo la Nakuru Daniel Mwangi alisema kuwa walilazimika kuvifunga vyoo hivyo kutokana na hali yake duni.