Wachuuzi wa vyakula katika mji wa Kisii na viungani mwake wameombwa kuzingatia usafi na kutotoroka wakati afisa wa afya wanapowatembelea.
wachuuzi hao pia wamehimizwa kuuzia vyakula vyao mahali pasafi kama njia moja ya kujali masilahi ya wateja wao.
Wakiongea siku ya Jumatatu walipotembelea wachuuzi hao katika soko kuu lililoko katikati mwa mji wa Kisii, wahudumu wa afya ya Jamii na wasimamizi wa afya kutoka hospitali kuu ya Kisii wakiongozwa na Kepha King’oina waliwaomba wachuuzi hao kuzingatia usafi na kuhakikisha kuwa mahali wanapouzia vyakula vyao ni pasafi kama njia moja ya kukinga wateja wao dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Aidha, wahudumu hao wa afya ya Jamii walisema kwa wachuuzi wengine hutoroka wakati wasimamizi wa afya katika kaunti ya Kisii wanapowatembelea kuona kama wanazingatia usafi jambo ambalo wamekashifu na kuwaomba wachuuzi hao kutotoroka.
“sisi kama wahudumu wa Afya ya Jamii lazima tuhakikishe kuwa kila kuchao kuna usafi na vyakula vinavyo uzwa mjini Kisii ni bora kwa wananchi," alihoji Kepha.
Wahudumu hao wa afya wakishirikiana na wasimamizi wengine wa afya kutoka hospitali ya Rufaa na mafunzo ya Kisii hutembea kila kuchao ili kuhakikisha kuwa vyakula vinavyopikwa na wachuuzi ni safi.
Wachuuzi hao walihimizwa kuhakikisha kuwa mahali wanapouzia ni pasafi na si karibu na barabara na nyumba zao lazima ziwe zimeidhinishwaa na sekta ya afya.
Wachuuzi hao pia wameobwa kuwa na barua kutoka hospitali ili kubaini hali yao ya afya.
Wasimamizi hao wa afya walisema kuwa watahakikisha kuwa wachuuzi hao wataweza kuendelea na biashara zao kwa njia ambayo inakumbalika.