Waendeshaji bodaboda katika mji wa Kisii na viungani mwake wameombwa kutoegesha pipikipi zao karibu na barabara na kuziba barabara hizo.
Wakiongea siku ya Jumatano katika mji wa Kisii, baadhi ya wakaazi na wahudumu wa Magari katika barabara pana inayoelekea hospitali ya Kibnafsi ya Hema na duka la jumla la Onshwa waliwaomba waendeshaji bodaboda hao kutoegesha pikipiki zao karibu na barabara bali waegeshe kando mwa barabara kwani wao husababisha msangamano wa magari.
“Najua vijana wetu wanatafuta riziki kama watu wengine lakini nawaomba kuegesha pikipiki zao mahali panapofaa wakati wanapowangojea wateja wao,” alisema James Kenani, mhudumu wa gari.
Aidha, walisema kuwa waendeshaji bodaboda hao hufunga baadhi ya njia katika mji wa kisii jambo ambalo huleta shida kubwa haswa wakati wa njioni watu wengi wanapotoka kazini.
Kwingineko, wasafiri wanaotumia miguu wamewaomba vijana hao kufuata sheria za barabara kwani waendeshaji bodaboda hao huwa hawawajali jambo ambalo huwaletea wasiwasi wanapovuka na kutembea katika mji wa Kisii.
“Naomba vijana hawa kufuata sheria za barabara na kupita mahali panapostahili kwani wao hawazingatii sheria hizo,” alisema Brian Osongo, mkaazi.
Kwa sasa wamewaomba vijana hao kuzingatia sheria hizo hili kupunguza ajali zinazotokana na pipkipiki hizo.
Pia wamewaomba kuwa na nidhamu kwani wakaazi hao wamedai kuwa waendeshaji bodaboda hao hutumia lugha ya matusi.
“Baadhi ya vijana hawa hawana nidhamu kwani hutumia matumizi mabaya ambayo ni ya aibu hata wakati mko na mtu wa heshima. Nawaomba kuwa na heshima ili sekta ya uchukuzi iweze kunawiri nanyi pia muweze kujiendeleza kimaisha,” alisema Dennis Ombaba, mkaazi.