Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa bodaboda katika mji wa Kisii wameombwa kuheshimu sheria za barabara zilizowekwa na serikali ya kaunti ya Kisii  na kutotumia baadhi ya barabara ambazo hawastahili kupitia.

kulingana na ratiba ya serikali ya kaunti ya Kisii, kuna baadhi ya barabara ambazo vijana hao hawastahili kupitia kwa ajili ya usalama na kuwepo na ofisi katika barabara hiyo kama njia moja ya kujiepusha na msongamano katika ofisi hizo.

Wakiongea siku ya Jumatatu katika barabara ya Mashauri-Kobil  karibu na ofisi kuu ya gavana wa Kaunti ya Kisii, wakaazi na polisi wa kaunti waliwaomba vijana hao kuheshimu sheria iliyowekwa. 

Aidha, walisema kuwa vijana hawa wakiheshimu sheria hiyo hakutakuwa na visa vya ajali wala polisi hawatakua wakibishana na nao kila wakati.

“Naomba vijana wetu kuheshimu sheria za barabara zilizowekwa ili sekta ya uchukuzi iweze kufanya kazi kwa urahisi, na tusiwe tunakimbizana nao kila siku," alisema mmoja wa askari wa kaunti ambaye hakutaka kutajwa kwa ajili ya usalma.

Kwingineko wakazi wa mji wa Kisii walisema kuwa sheria hiyo imesaidia pakubwa kwani kuna ofisi nyingi za serikali kuu na serikali ya kaunti katika barabara hiyo na kwa sasa wanafika katika ofisi hizo bila shid yoyote.

“Siku hizi tunafika katika ofisi ambazo ziko katika barabara hii kwa urahisi na naomba vijana hawa waweze kuheshimu sheria hiyo,” alisema Evans Nyachoka, mkaazi.