Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wafanyibishara rejareja katika mji wa Kisii wameombwa kuzingatia usafi na kuwa na uwazi wanapouza bidhaa zao.

Baadhi ya wanaonunua bidhaa kutika kwa wafanyibiashara hao walidai kuwa baadhi ya hao watu huwatapeli kwa kuwadanganya kuwa baadhi ya vitu wanaowauzia vina uwezo wa kuwapa huduma zingine, lakini sio ukweli.

Wachuuzi hao ambao ni wakuzunguka katika mji wa Kisii wakiziuza bidhaa zao sasa wameombwa kufanya biashara zao kwa uwazi na kuuza biadha ambazo zinazokubalika kwani kuna baadhi yao wanauza bidhaa ghushi kwa wateja wao.

Aidha, wameombwa kuzingatia usafi kila mara kwa kuwa wamekuwa wakionekana wakitupa uchafu popote katika mji huo, jambo ambalo linawakera wengi huku wakionywa kuwa watachukuliwa hatua ya kisheria kwa kuchafua mazingira.

Wakiongea katika kituo cha magari mjni Kisii, wakazi hao waliwaomba watu hao kuwajibika kazini kwa kuwa visa vya utapeli vimeripotiwa huku wafanyi biashara wa aina hiyo wakihusishwa.

Kwa sasa wamewaomba wafanyibiashara hao kushirikiana na serikali kuwachunguza wenzao ambao wamejiunga katika kazi hiyo huku nia yao ikiwa ya kuwatapeli watu ili waweze kutambuliwa na kuchukuliwa hatua ya kisheria.

Kwa upande wa usafi mwenyekiti wa kikundi cha kufanya usafi katika mji wa Kisii Kepha King’ona aliwaomba watu hao kuzingatia usafi kila mara kwani ni wajibu wa kila mtu kuzingatia usafi mahali wanapofanyai kazi.

King’ona aliwaomba wafanyibishara kujua umuhimu wa kuwa na uwazi uwepo katika biashara kati ya mteja wake kwani biashara lazima iwe na pande hizo pili.