Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyibiashara wa ndizi katika soko la Daraja Mbili mjini Kisii wameiomba serikali ya kaunti hiyo kuwatafutia soko ya mazao yao, ili kukuza biashara hiyo na kuinua uchumi wa kaunti.

Ombi hilo limetolewa baada ya serikali ya kaunti kuwaahidi wafanyibiashara na wakulima wa ndizi kuwa ndizi zao zingenunuliwa kutoka kwao na serikali ya kaunti, jambo ambalo wanalisema limekawia kuafikiwa kikamilifu.

Kulingana na wafanyibiashara hao, huwa wanapata hasara nyingi kwa kusafirisha vyakula hivyo kutoka makwao, huku wengi wakilalamiakia usafiri na bei duni.

Wakiongea na mwandishi huyu siku ya Alhamisi katika soko hilo wafanyibiashara hao wakiongozwa na Susan Onsano walisema soko ya ndizi imeadhirika kwa kiasi kikubwa kufuatia kuvunwa kwa mahindi, na kusema wanaendelea kukadiria hasara kubwa.

“Kila siku tangu mwezi wa saba tunatozwa ushuru na hakuna soko ya ndizi, huwa tunakadiria hasara nyingi ya uchukuzi, kununua kutoka kwa wakulima, kutozwa ushuru na bei ya ndizi ni duni,” alisema Onsiemo, ambaye pia ni mfanyibiashara.

“Tunaomba serikali jinsi ilituahidi hapo mbeleni kuwa ingetutafutia soko au kununua kutoka kwetu tumekuwa tukisubiri kwa mda mrefu sasa na tunaomba tutafutiwe soko ya ndizi," aliongezea.